Kitabu cha sekondari cha Longhorn, kitabu cha mwanafunzi, kidato cha tatu, kimeandikwa kwa utondoti kwa kuzingatia mahitaji yote ya silabasi ya kidato cha tatu. Wandishi wa kitabu hiki ni walimu wenye tajriba pana ya ufundishaji wa lugha ya Kiswahili darasani. Wamefundisha Kiswahili kwa ngazi tofauti za elimu nchini Uganda kama vile; shule za sekondari, vyuo vya walimu wa shule msingi na za sekondari, vyuo vikuu kwa miaka mingi. Mwanafunzi atakayekisoma kwa makini na kufuata maagizo yaliyomo atajifunza Kiswahili kwa urahisi na kupata umilisi ulionuiwa.